Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NIMR yafanya utafiti dawa ya kutibu tezi dume

Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Profesa Pascal Ruggajo akizungumza na wataalamu mbalimbali kwenye Kongamano la pili la Kisayansi la Tiba asilia lililofanyika Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Ni hatua nyingine kwa Serikàli, hii ni  baada ya kuwatangazia wananchi  kuwa sasa wanaweza kuchagua aina ya dawa katika Hospitali saba nchi (asilia au ya kisasa) atakayopewa baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika na ugonjwa.

Dar es Salaam. Ni faraja kwa wagonjwa wenye tatizo la uvimbe wa tezi dume, hii ni baada ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kusema, inakamilisha utafiti wa dawa kushugulikia tatizo hilo kwa wanaume.

Dawa hiyo itakayokuwa na jina la NIMR genic inatafitiwa kubaini namna ya kuzuia uvimbe wa tezi dume au kutibu tatizo hilo.

Japo tafiti mbalimbali zinaonyesha uvimbe wa tezi dume hushambulia wanaume kuanzia miaka 40,  kuongezeka kwa kiungo hicho ni kutokana na vichocheo vya homoni katika mwili ambavyo vinasababisha tezi dume kukua na kuathiri kibofu cha mkojo.

Dawa hiyo itatolewa hospitalini kwani tayari wizara ya afya imetangaza dawa za asili takribani 19 za maradhi mbalimbali kutolewa katika Hospitali 17 za umma.

Hayo yameelezwa leo Agosti 30, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR  Profesa Said Aboud katika kongamano na pili la wataalamu wa tiba asili ikiwa ni siku moja kabla ya Maadhimisho ya Siku ya Tiba ya Asili kwa Mwafrika.

"NIMR Genic inafanyiwa utafiti kwa ajili ya uvimbe wa tezi dume, watoa huduma wote wa tiba asili wafike NIMR na dawa zao tuzifanyie utafiti kuangalia dawa zao kama ni salama,” amesema.

Dawa nyingi bado tunaendelea kuzifanyia tafiti na zingine tayari tumeshazifanyia ikiwemo NIMR CAF, Bupiji na mengine," amesema.

Akifungua mkutano, Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Profesa Pascal Ruggajo amesema Serikàli imeendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya afya na kuendeleza matibabu ya asili.

"Miongoni mwa vipaumbele vya Wizara ya Afya ni ukuzaji na uendelezaji wa tafiti za tiba asilia tayari katika Hospitali saba nchini dawa 19 zinatolewa baada ya wataalamu wa afya kwenye hospitali hizo kujengewa uwezo," amesema.

Amesema dawa za asili zimekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania hasa kipindi cha uviko -19 nchi mbalimbali zilipitia changamoto nyingi lakini athari hizo kwa kiwango kikubwa hazikuonekana hapa nchini kutokana na matumizi ya dawa hizo.

"Sasa mgonjwa akienda kwa daktari anaweza kupimwa na kuambiwa ugonjwa wake na kuchagua aina ya dawa anavyotaka kutumia, tayari tuna dawa za pumu, vidonda vya tumbo na mengine ambayo itatolewa katika hospitali zetu 17  baadhi ni Sekotoure, Temeke, Simiyu na Bombo mkoani Tanga,"amesema.

Kaimu Mkurugenzi a Tiba asilia Wizara ya Afya, Dk Vumilia Liggie amesema, dawa za asilia katika hospitali za umma zitaendelea kuongezeka kulingana na tafiti zinazofanyika.

"Zipo dawa zinatiba matatizo ya hedhi, kuchomwa na moto na magonjwa ya upumuaji na tayari wataalamu wa afya 21 tumewajengea uwezo na tunawatambua wazalishaji wandawa zaidi ya 43,000 kote nchini," amesema.

Mmoja wa wazalishaji wa dawa asilia, Mussa Daudi kutoka Arusha amesema kwa sasa Tanzania huduma ya tiba asilia imekuwa huduma muhimu.

Kongamano hilo la pili la dawa asilia limewakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo watunga sera, watumiaji wa dawa, watengenezaji na wanasayansi.