Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyara za wapeleka jela miaka 25

Muktasari:

Hakim  Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ismail Ngaile juzi aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Marwa Nyamhanga (47), Paulo Ryoba (50), Rhobi Chacha (30) na Machoni Marwa wa kazi wa Wilaya ya Serengeti.

 Serengeti. Mahakama ya Wilayaya Serengeti imewahukumu watu wane kifungo cha miaka 25 jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne likiwamo la kumiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Hakim  Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ismail Ngaile juzi aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Marwa Nyamhanga (47), Paulo Ryoba (50), Rhobi Chacha (30) na Machoni Marwa wa kazi wa Wilaya ya Serengeti.

Kabla ya hukumu, Ngaile alisema mshtakiwa wa kwanza, Nyamhanga amepatikan ana makosa ya kuhujumu uchumi, kuingia hifadhini bila kibali, kukutwa na kisu na nyaya za kutegea wanyama

Mshtakiwawa pili, watatu na wane walipatikana na makosa ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kukutwa na kisu, nyaya za kutegea wanyama na ngozi ya swala yenye thamani ya Sh877,500.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Emmanuel Zumba alidai washtakiwa hao walikamatwa Juni 4 mwaka jana saa 11:30 jioni, eneo la Tenyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.