Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyumba yaangukiwa na udongo Same, wanafunzi wawili wafa

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema waliofariki dunia ni Rahel Elireema (13) mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Myamba na Rahel Elirehema(7) mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Myamba

Same. Wanafunzi wawili wa familia moja wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro, wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Januari 31, 2024 baada ya nyumba yao kuangukiwa na udongo wakati wamelala.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa vifo vya Rahel Elireema (13) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Myamba na Rahel Elirehema (7) mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Myamba.

"Ni kweli kumetokea vifo vya watoto wawili ambao wameangukiwa na gema wakati wamelala kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Same na Mkoa wa Kilimanjaro kwa jumla," amesema Babu.

Pia,  amesema kwa sasa kutokana na mvua zinazoendela kunyesha wilayani humo barabara zimeharibika na hazipitiki, huku akiagiza kamati ya maafa ya wilaya kwa kushirikiana na Tarura wilayani humo kufika katika maeneo hayo.

Akizungumza na Mwananchi Digital, kaka wa watoto hao, Youze Elirehema amesema gema la udongo liliangukia nyumba iliyokuwa na watu wanane wamelala wakiwamo baba, mama na ndugu wengine wanne ambao wamenusurika na wawili ambao wamefariki dunia.

"Ilikuwa saa nne ya usiku jana, nilipata taarifa kuwa nyumbani kuna matatizo, kwamba wadogo zangu wamefukiwa na gema la udongo, nilipofika nilikuta nyumba imeanguka na wadogo zangu wawili wamefariki na wanne walisalimika," amesema Elirehema.

"lilishuka gema la udongo likavunja nyumba likaingia ndani na wakati huo mtoto mmoja alikuwa amelala na mwingine alikuwa anajisomea, huyu alibanwa na meza tumboni baada ya kuangukiwa na gema, wakati anaomba msaada  kuokolewa likamwangukia gema lingine na kufariki hapo hapo.”

Amesema familia wamepata pigo kubwa kwa kuondokewa na watu wawili kwa wakati mmoja.