Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyumba zaidi ya 120 zaharibika Zanzibar

Muktasari:

Kaimu Mkurugenzi Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu, Aprili 16 amesema kuwa takwimu hiyo ni ya awali tu ila wanatarajia  huenda ikaongezeka zaidi kutokana na maeneo mengi bado hayajafanyiwa uhakiki.

Zaidi ya nyumba 120 zimeharibika vibaya katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa muda wa siku mbili mfululizo.

Kaimu Mkurugenzi Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu, Aprili 16 amesema kuwa takwimu hiyo ni ya awali tu ila wanatarajia  huenda ikaongezeka zaidi kutokana na maeneo mengi bado hayajafanyiwa uhakiki.

Amesema miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika na mvua hizo ni pamoja na Amani Kwawazee, Daraja Bovu, Seblen, Mwanakwerekwe, Fuoni pamoja na Kibonde Mzungu.

Amesema mbali ya maeneo hayo lakini pia kuna baadhi ya miundombinu ya barabara nayo imeharibika ikiwamo barabara ya Fuoni pamoja na Mwanakwerekwe ambayo imefungwa kabisa kutokana na kujaa maji maeneo yote na kusindikana vyombo vya moto pamoja na wananchi kushindwa kupita.

Amesema hivi sasa wanaendelea kukusanya taarifa kutoka kila pande ya miji ya Zanzibar ili kujua athari kwa ujumla pamoja na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na maafa Zanzibar.