Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa wa Polisi na wenzake wadaiwa kuiba Sh600, 000

Muktasari:

  • Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Lidya Ngua na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la wizi wa Sh600, 000.

Dar es Salaam. Watu watano akiwemo Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Lidya Ngua wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la wizi wa Sh600, 000.

Akisoma hati ya mashtaka leo Machi 14, Wakili wa Serikali, Caroline Matemu amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kumuibia Sofia Liana Mbaga.

Matemu amedai kuwa kati ya Februari 21, 2020 eneo la Charambe Kisutu wilayani Ilala washtakiwa hao walimwomba Sofia Mbaga kiasi cha Sh600, 000.

Amesema upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu Amir Msumi alisema ili washtakiwa hao wadhaminiwe ni lazima kila mmoja awe na mtu mmoja atakayesaini bondi ya Sh 600,000.

Washtakiwa hao walikidhi masharti ya dhamana hiyo na wapo nje kwa dhamana na kesi imeahirishwa hadi Machi 23, 2023 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.