Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ole Sabaya, IGP Sirro kuwa mashahidi kesi ya Mbowe

Ole Sabaya, IGP Sirro kuwa mashahidi kesi ya Mbowe

Muktasari:

  • Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, wanatarajia kuwa mashahidi kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, wanatarajia kuwa mashahidi kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake watatu kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kudaiwa  kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya  Hai, Lengai Ole Sabaya.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2020, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala, baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomewa washtakiwa hao, maelezo ya mashahidi, idadi ya mashaidi na idadi ya vielelezo.

Kibatala ameieleza Mahakaka hiyo mbele ye Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo( Commital Proceedings).

" Mheshimiwa Hakimu Hakimu, upande wetu wa utetezi tunatarajia kuwa na mashahidi wawili ambaoni IGP Sirro na Lengai Ole Sabaya," amedai Kibatala.