Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Olengurumwa: Tunapaswa kuangalia mifumo ambayo haitaleta madhara ya kupambana na uhalifu

Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa.

Muktasari:

  • Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa licha ya kupongeza ripoti iliyowasilishwa amebainisha baadhi ya maeneo hayakaa sawa na ameshauri yanapaswa kuendelea kufanyiwa kazi.

Dar es Salaam. Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa licha ya kupongeza ripoti nzuri iliyowasilishwa na Tume ya kuchunguza haki jinai nchini amesema kuna baadhi ya maeneo hayajakaa sawa.

Ngurumwa ameyabainisha leo Jumatano, Julai 19, 2023 kwenye mjadala wa Mwananchi Twitter Space uliokuwa na mada ya ‘Je, yaliyopendekezwa na Tume ya haki jinai yanakidhi haja?’

Ametolea mfano adhabu ya kifo ambapo amedai tume hiyo imependekeza iwe na kikomo huku akielezwa kwakuwa haitekezwi ameshauri ibadilishwe.

“Kwakuwa sheria ya kifo haijawahi kutekelezwa ni muhimu ikabadilishwa iwe na miaka angalau 70 au 50 huyu akitoka hapo amejifunza hatakuwa na madhara kwenye jamii. Tunapaswa twende mbele kama taifa kuangalia mifumo ambayo haitaleta madhara ya kupambana na uhalifu,” amesema 

Pia, Ngurumwa amesema wakati wanatoa maoni yao kwa tume hiyo walipendekeza Jeshi la Polisi liitwe vyuo vya mafunzo ili watambue wanajukumu la kuwahudumia Watanzania na si kazi yake kupambana na raia.

“Dhana ya Jeshi la Polisi watu wanaamini lipo kwa ajili ya kundi fulani na kuzuia uhalifu ni lazima jamii husika iwe sehemu, jamii iwe na mahusiano mazuri ya vyombo vya usalama la kulinda jamii. Uhalifu hauwezi kutokomezwa kama hakuna uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na Rais,” amesema 

Katika kukazia hoja hiyo amesema asilimia kubwa ya falsafa na dhana zilizojengeka ni zile za kikoloni na kwamba bado mambo mengi yanatekelezwa kwa dhana zilizotumika na wakoloni.

“Mifumo kwa ajili ya kumkandamiza yule anayetawaliwa, sisi tulipeleka maoni kwamba hayo yaondolewe, dhana hiyo inajengeka kwahiyo tuangalie taasisi zote Magereza,” amesema 
Mwishooo