Padre Haule wa St Peters afariki dunia

Padre Haule wa St Peters afariki duniani

Muktasari:

  • Ni mkurugenzi wa matangazo wa Radio Tumaini aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro jijini Dar es Salaam, Padre Paul Haule amefariki dunia leo saa 10:30 jioni wakati akitibiwa katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyopo Ukonga.

Kumekuwa na taarifa inayozunguka mtandaoni iliyoandikwa na Padre Vincent Mpwaji ikibainisha kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa.

Padre mmoja ambaye si msemaji wa msiba huo amelithibitishia Mwananchi kuhusu kifo cha Padre Haule.

“Alilazwa kwa siku kadhaa sijabahatika kujua ni ngapi lakini ametutoka na hivi tunavyozungumza mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo,” amesema padre huyo.

Mbali na kuwa paroko msaidizi, Padre Haule alikuwa mkurugenzi wa matangazo Radio Tumaini.