Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Padri aliyeuawa Mbeya kuzikwa leo

Muktasari:

  • Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Gervas Nyaisonga amewaongoza waumini katika ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Padri wa kanisa hilo wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Michael Samson aliyeuawa Juni 11.


Mbeya. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Gervas Nyaisonga amewaongoza waumini katika ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Padri wa kanisa hilo wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Michael Samson aliyeuawa Juni 11.

Padri Samson raia wa Malawi aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwakatwa mapanga na viungo vyake kutengenishwa huku mwili wake kutupwa katika Mto Meta maeneo ya Sabasaba jijini humo, ambapo leo Alhamisi Juni 16 anatarajiwa kuzikwa katika makaburi yaliyopo Mwanjelwa.

Katika ibada hiyo, mbali na Askofu huyo pia viongozi wa serikali akiwamo Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa ni miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ambayo inaendelea katika Kanisa hapo.

Akizungumza wakati wa ibada hiyo, Askofu Nyaisonga amewaomba wananchi kutoka mataifa ya Tanzania, Malawi na Zambia kushirikiana na Mamlaka katika kusaidia uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo.

Amewaomba waumini kupokea msiba huo kiimani akieleza kuwa kwa sasa ni kumuombea marehemu kupumzika kwa amani na kupokelewa na Mungu akibainisha kuwa tukio hilo limehusisha mtu au watu.

"Hiki kitendo kimefanywa na mtu au watu, lakini ili roho ya marehemu iwe na amani na sisi tuliobaki pamoja na ndugu zake, naomba tushirikiane na mamlaka kufichua waliotenda unyama huu ili haki ipatikane, kifo cha Padri ni fumbo kwetu," amesema Askofu huyo.