Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tabora wakamata magari 1000 kwa makosa mbalimbali

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekamata magari zaidi ya 1000 katika muda wa siku 11 katika operesheni iliyoendeshwa Aprili 4 hadi 15 mkoani humo.

Tabora. Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekamata magari zaidi ya 1000 katika muda wa siku 11 katika operesheni iliyoendeshwa Aprili 4 hadi 15 mkoani humo.

Akizungumza leo Jumamosi Aprili 16, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema wamekamata magari 455 mabovu, 164 kwa kosa la kuzidisha abiria, 392 kwa kuendesha  mwendo kasi, 281 kutokuwa na stika za ukaguzi na madereva wa magari 36 wamekamatwa kwa kosa la kutokuwa na leseni.

"Tunajaribu kupunguza makosa yanayofanywa barabarani na ndio maana tumefanya operesheni hii” amesema

Kamanda Abwao amesema wamekamata madereva wa bodaboda 75 kwa kosa la kutovaa kofia ngumu pamoja na 58 kwa kubeba abiria zaidi ya mmoja.