Polisi walivyotinga kupekua nyumbani kwa Boni Yai
Muktasari:
Msafara wa magari ya polisi uliombeba aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob maarufu ‘Bon Yai’ ukiwasili nyumbani kwake Mbezi Msakuzi kwa ajili ya upekuzi.
Dar es Salaam. Msafara wa magari ya polisi uliombeba aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob maarufu ‘Bon Yai’ ukiwasili nyumbani kwake Mbezi Msakuzi kwa ajili ya upekuzi.
Msemaji wa Polisi, David Misime amesema wanamshikilia kwa makosa mbalimbali ya jinai.
“Jeshi la Polisi limemkamata na linamshikilia Boniface Jacob, mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi, jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo.
“Hivyo, wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo, David Misime.
Taarifa za Jacob kukamatwa, zimeanza kusambaa mitandaoni leo Septemba 18, 2024 mchana kwamba amekamatiwa Sinza, jijini Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia Mwananchi