PPRA yaanza kushirikisha wenye ulemevu kuomba zabuni kwenye miradi

  • Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya umma(PPRA) imeanza kuwajengea uwezo wajasiliamali  wenye Ulemavu wa kusikia ili waweze kushiriki kwenye michakato ama miradi mbalimbali ya Zabuni inayotolewa na Serikali.(Picha Lilian Lucas).

Muktasari:

  • Katika kuhakikisha makundi maalumu nchini yanashiriki katika suala la kuomba zabuni zinazotolewa au kutangazwa na mamlaka mbalimbali za Serikali, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeanza kuwajengea uwezo wajasiliamali wenye ulemavu wa kusikia ili waweze kushiriki kwenye michakato mbalimbali ya zabuni na kupata.

Morogoro. Katika kuhakikisha makundi maalumu nchini yanashiriki katika suala la kuomba zabuni zinazotolewa au kutangazwa na mamlaka mbalimbali za Serikali, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeanza kuwajengea uwezo wajasiliamali wenye ulemavu wa kusikia ili waweze kushiriki kwenye michakato mbalimbali ya zabuni na kupata.


Kundi hilo la wenye ulemavu wa kutosikai linapata mafunzo ya sheria ya ununuzi na lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutengeneza zabuni zenye kukidhi viwango na matakwa ya kisheria.


Kaimu mkurugenzi mkuu wa PPRA, Marry Swai akizungumzia sheria ya ununuzi kwa wenye ulemavu kwenye warsha inayoendelea mkoani Morogoro, alisema kuwa lengo kuu ni kufundisha kundi hilo taratibu wanazotakiwa kufuata, namna ya kutengeneza zabuni ambazo zinakidhi matakwa ya sheria.

“Ili uweze kuingia kwenye mchakato wa zabuni lazima ujue sheria inakutaka ufanye nini, unavyojaza kabrasha unatakiwa ujazeje ili hatimaje zabuni iweze kuonekana iko kwenye ushindani ili ushinde na bila kufanya hivyo kutakuwa hatuwatendei haki kwa sababu hamtaweza kushiriki,”alisema.


Swai alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi lakini kuwepo kwa changamoto hizo ni fursa ni kwamba kufahamika kwake kunawezesha kupata fursa ya kushiriki kwenye zabuni zinzotangazwa na Serikali kwa kujari makundu yote.


Aidha alisema Serikali ni sikivu na imekuwa ikijali makundi yote ndio maana imeweka kipenge maalumu kwenye sheria yake na inatakiwa kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kwa ajili ya makundi maalumu.


“Katika makundi maalumu halitashindanishwa na makundi maalumi, itatoka zabunii na kutangazwa hivyo watu ambao hawana ulemavu hawataruhusiwa kushiriki kwa mujibu wa sheria,”alisema Swai.

Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA), Calvin Mnyema alisema kutolewa kwa mafunzo hayo kutasaidia na kuwajengea ujasili wa kuomba zabuni kwani jamii ya viziwi wengi ni wajasiliamali na wafanyabiashara hivyo ni muhimu kupata mafunzo ili waweze kuelewa sheria ya manunuzi ya Umma.


“Hapa kuna washonaji, wajasiliamali kwa hiyo mafunzo haya yatatujengea uwezo kufahamu njia gani ya kuweza kununua vifaa mbalimbali kwa sababu PPRA wanatufundisha sheria hii na viziwi wana hamu ya kufahamu,”alisema.   


Alisema wapo baadhi ya viziwi wanataka na kutambua wanaweza kununua wapi vifaa ili wasipate shida wakati wanapohitaji mahitaji pindi watakapopata zabuni.


Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Jesca Kagunila aliwataka viongozi wa Tamavita kuendelea kuhamasisha wanachama wao na wale wasiowanachama kuchangamkia fursa za zabuni ambazo zimekuwa zikitangazwa ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.