Profesa Mkenda ataka wenye ulemavu washirikishwe Sensa
Muktasari:
- Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka wananchi wa Wilaya ya Rombo kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23, 2022
Rombo. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka wananchi wa Wilaya ya Rombo kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23, 2022
Profesa Mkenda ambaye ni Mbunge wa Rombo amewataka wananchi wa Wilaya ya Rombo kushiriki kikamilifu katika sense.
Ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 15, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mamsera, wilayani humo.
"Naomba Rombo yote tuhesabiwe na wenye ulemavu wa aina yoyote mhakikishe na wao wanahesabiwa, ukimficha ndani atakosa huduma muhimu za kijamii maana akiwa na changamoto kubwa tutampeleka hata shule za bweni, hakuna kumficha mtoto ndani," amesema Profesa Mkenda
Profesa Mkenda ameeleza umuhimu wa sense na kuwataka wananchi wa wilaya hiyo wajitokeza kwani watakaokwepa watasababisha kukosekana kwa huduma muhimu.