Putin atangaza operesheni ya kijeshi kwa Ukraine

Muktasari:

  • Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza operesheni ya kijeshi katika eneo la Donbas nchini Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza operesheni ya kijeshi katika eneo la Donbas nchini Ukraine.

Akitoa tamko hilo katika hotuba ya televisheni Alhamisi asubuhi amewataka wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano mashariki mwa Ukraine kuweka silaha chini na kurejea majumbani mwao.

Saa chache baadae milipuko ilisikika katika miji ya Odessa, Kharkiv, Kramatorsk, Mariupol and Kyiv

Naye Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema operesheni ya Russia imelenga kambi za jeshi za taifa hilo.

Nchi nyingi duniani zikiwamo Marekani zimeikosoa vikali hatua hiyo ya Russia kuivamia Ukraine.