Raila Odinga apiga kura, wafuasi wamlaki

Mgombea urais wa tiketi ya Azimio La Umoja, Raila Odinga akipiga kura kwenye kituo cha shule ya msingi Old kibera.

Muktasari:

Mgombea urais wa tiketi ya Azimio La Umoja, Raila Odinga leo saa 4.30 asubuhi amepiga kura kwenye kituo cha shule ya msingi Old kibera huku akilakiwa na wafuasi wengi barabarani huku wakiimba nyimbo za kumshangilia.

Nairobi. Mgombea urais wa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga leo saa 4.30 asubuhi amepiga kura kwenye kituo cha shule ya msingi Old kibera huku akilakiwa na wafuasi wengi barabarani huku wakiimba nyimbo za kumshangilia.
Odinga aliyekuwa ameambatana na wasaidizi wake na mke wake wamefanikiwa kupiga kura huku wafuasi wake wakiendelea kupiga kura kwenye kituo hicho.
Baada ya kupiga kura mgombea huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha ODM hakuongea neno lolote, alipanda kwenye gari na kuondoka lakini mke wake Ida Odinga amesema kuwa kazi iliyobaki ni Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa wakweli kwenye utoaji wa matokeo.
“Wapiga kura wanafanya kazi yao, kilichobaki ni kwa Tume (IEBC) kufanya kazi yao kwa ukweli na weledi. Najisikia furaha leo kupiga kura,”
Hata hivyo wapambe wa waziri mkuu mstaafu, Raila Odinga mpaka mgombea huyo anaondoka eneo hilo walikuwa wakilalamikia mfumo wa kieletroniki wa kupiga kura (Kiems) kuwa na matatizo na wanahofia wengi hawatapiga
“Mimi nimekuja hapa kumsindikiza Baba (Odinga) na mke wake lakini tunashukuru Baba amepiga kura ila sisi bado mfumo wa kiems unatusumbua,” amesema Esther ambaye ni mfuasi wa Azimio la Umoja.