Rais Kenyatta awatoa hofu Wakenya

Muktasari:

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amepiga kura leo katika kituo cha Shule ya msingi Motomo iliyopo katika jimbo la Gatundu akiwa akiwa na mkewe Margaret Kenyatta

Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amepiga kura leo katika kituo cha Shule ya msingi Motomo iliyopo katika jimbo la Gatundu akiwa akiwa na mkewe Margaret Kenyatta
Uhuru alifika katika kituo cha kupigia kura na alitumia muda mfupi katika mashine ya utambuzi kama ni mpigakura wa eneo hilo ambapo alikuwa akiongozwa na msimamizi wa kituo husika
Baada ya kukamilisha taratibu za utambuzi alipewa karatasi za kura na kwenda kupiga kwenye eneo maalumu lililotengwa kwa shughuli hiyo, kiongozi huyo ametumia takriban dakika 5 hadi kukamilika.
Mara baada ya kupiga kura, Kenyatta amezungumza na waandishi wa habari ambapo amesema upigaji kura umekwenda vizuri katika eneo lake na aamini utakuwa hivyo kwa nchi nzima
Amesema Wakenya watapiga kura kwa amani, utulivu na kwenda majumbani kwao kusubiri matokeo ambayo yatatangazwa kulingana na taratibu zilizopo chini ya usimamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) na Mipaka.