Rais Samia ataka tathmini upya utatuzi migogoro ya ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akizungumza mkoani Morogoro katika ufunguzi wa kikao maalumu cha wadau  wa Ardhi na Viongozi wa mkoa huo 

What you need to know:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ametaka tathmini kufanyika upya katika utekelezaji wa taarifa ya uamuzi wa baraza la mawaziri juu ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.


Morogoro. Rais Samia Suluhu Hassan ametaka tathmini kufanyika upya katika utekelezaji wa taarifa ya uamuzi wa baraza la mawaziri juu ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Kauli hiyo ya Rais Samia imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dk Angelina Mabula katika utekelelezaji wa mapendekezo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwenye kikao maalumu cha wadau  wa ardhi na viongozi wa Mkoa wa Morogoro.

Dk Mabula amesema baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa yanapaswa kupitiwa upya kutokana na kupita muda mrefu bila kutolewa uamuzi wa maeneo yaliyotolewa na serikali na wananchi kuvamia bila kufuata taratibu pamoja na yaliyopendekezwa kuchukuliwa na wananchi yakionekana kutofaa tena kwa uhifadhi.

Waziri huyo pia akatoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, taasisi mashirika,  mbalimbali kuhakikisha wanalinda vyema ardhi yao kwa kuwa jukumu la ulinzi wa ardhi ni la kwako mwenyewe.