Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua, ahamisha, atengua


Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Desemba 18, 2023 amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa vituo vya kazi vya watumishi mbalimbali wa Serikali wakiwamo wakurugenzi wa halmashauri, balozi na mwenyekiti wa bodi.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema, Rais Samia amemteua Balozi Meja Jenerali Paul Simuli kuiwakilisha Tanzania nchini Uganda.

Aidha, amemteua Selwa Hamid kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Igunga akichukua nafasi ya Francis Msabila aliyesimamishwa kazi.

“Amemteua Mariamu Chaurembo kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Mji Tunduma akichukua nafasi ya Lena Nkya ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

“Amemteua Fabian Said kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Momba, akichukua nafasi ya Butamo Nuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, amemuhamisha kituo cha kazi Dk Peter Nyanja aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba na kwenda Halmashauri ya Wanging’ombe, Dk Nyanja anachukua nafasi ya Maryamu Muhaji ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Manyara.

Pia, Rais Samia amemteua Dk Khamis Mwinyimvua kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Dk Mwinyimvua ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Profesa Longinus Rutasitara aliyemaliza muda wake.