Rais Samia ateua Ma-DC wapya 37, apangua 48

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amepangua ya wakuu wa wilaya ambapo jumla ya wakuu wa wilaya 47 kote nchini wamehamishwa vituo vyao vya kazi.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 37 na kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 huku 55 wakibaki kwenye nafasi zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 25, 2023 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amefanya mabadiliko hayo na kuwateua wakuu wa wilaya wapya 37 huku wengine 47 wakihamishwa vituo vya kazi.

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vyao vya kazi ni Suleiman Mwenda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba sasa atakuwa mkuu wa wilaya ya Monduli, mwingine ni Edward Mpogolo aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Same sasa atakuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala.

Naye Halima Bulembo  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza sasa ataongoza Wilaya ya Kigamboni, Hashim Komba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea sasa ataiongoza Wilaya ya Ubungo.

“Mwanahamisi Mukunda aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Bahi sasa ni Mkuu wa wilaya Temeke, Saadi Mtambule aliyekuwa Mkuu wa wilaya Mufindi amehamishiwa wilaya ya Kinondoni, naye Sophia Kizigo aliyekuwa Mkuu wa wilaya Mkalama amehamishiwa wilaya ya Mpwapwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Godwe atakuwa Mkuu wa wilaya ya Bahi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Misungwi Veronica Kessy atahudumu wilaya ya Iringa.

Kwa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Nzega ACP Advera Bulimba ataongoza Wilaya ya Biharamulo huku Majid Mwanga aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa ataiongoza wilaya Mlele.

“Mkuu wa wilaya ya Magu, Salum Kali naye amehamishiwa wilaya ya Kigoma, Kisare Makori aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Uyui atakukuwa Wilaya ya Moshi, Mohamed Moyo aliyekuwa Wilaya ya Iringa atakuwa Mkuu wa Wilaya Nachingwea,” ilielezwa kwenye taarifa hiyo.

Wengine ni Kherry James aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo sasa ataiongoza wilaya ya Mbulu, Dk Vicent Anney amehamishwa kwenda Wilaya ya Bunda akitokea Wilaya ya Rungwe na Kanali Denis Mwila amepelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya Mbarali akitokea Wilaya ya Ukerewe.

Mabadiliko hayo pia yamemgusa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawaga Sebastian Waryuba ambaye sasa kituo chake cha kazi ni Wilaya ya Malinyi, Danstan Kyobya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara sasa atahudumu kwenye nafasi hiyo kama Mkuu wa wilaya ya Kilombero.

Pia Dk Julius Ningu amehamishiwa Wilaya ya Ulanga akitokea wilaya Namtumbo naye Judith Nguli amehamishiwa Wilaya ya Mvomero akitokea Wilaya ya Liwale, Hanafi Msabaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

“Luter Kanoni atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Wanging’ombe, Matiko Chacha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua atahudumu Wilaya Misungwi, Ng’wilabuzu Ludigija aliyekuwa Wilaya ya Ilala sasa atahudumu wilaya ya Kwimba, Claudia Kitta kutoka Wilaya ya Masasai sasa atakuwa wilaya ya Wanging’ombe akitokea wilaya ya Masasi,” mabadiliko hayo yanaonyesha.

Aliyeguswa mwingine, Fatma Nyangasa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni sasa ni ataiongoza Wilaya ya Kisarawe na Nick John aliyekuwa wilaya hiyo amehamishiwa Wilaya ya Kibaha na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Halima Okash ataiongoza wilaya ya Bagamoyo.

Vilevile Filberto Sanga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mlele atahudumu Wilaya ya Nyasa na Ngollo Malenya aliyekuwa wilaya Ulanga sasa atakuwa Namtumbo, Simon Simalenga aliyekuwa Wilaya ya Songwe atahudumu wilaya ya Bariadi.

“Johari Samizi aliyekuwa wilaya ya Kwimba atahudumu wilaya Sinyanga,Anna Gidarya atahudumu wilaya ya Busega akitokea wilaya Ileje,Mosses Machali aliyekuwa wilaya Bukoba atahudumu wilaya Mkalama na Thomas Apson amehamishiwa wilaya ya Ikungi akitokea Siha,” alifafanua taarifa hiyo.

Mkeka huo pia umemgusa Kemilembe Lwota aliyekuwa Wilaya ya Biharamulo na sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Joshua Nassari aliyehudumu Wilaya ya Bunda sasa ataendelea kuhudumu kwenye nafasi hiyo wilayani Iramba na Esther Mahawe amehamishwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbozi akitokea wilaya ya Kigoma.

Pia Simmon Chacha aliyekuwa wilaya ya Sikonge sasa ataiongoza wilaya ya Sikonge, Said Mtanda aliyekuwa Wilaya ya Arusha sasa atahudumu Wilaya ya Urambo na Dk Mohamed Chua chua aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Mbeya atahudumu Wilaya ya Kaliua.

Louis Bura atahudumu wilaya ya Tabora akitokea wilaya ya Urambo na Jokate Mwegelo aliyekuwa Wilaya ya Temeke sasa atahudumu Wilaya ya Korogwe, naye Albert Msando aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Morogoro amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni,

Pia Juma Irando amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza akitokea Wilaya ya Hai na Zainab Issa aliyekuwa Bagamoto sasa atahudumu Wilaya ya Pangani.

Wanaoendelea kubaki kwenye nafasi hizo ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatu Dadi Kolimba, Raymond Mangwala (Ngorongoro), Dk Khamis Mkanachi (Konda) na Remedeus Emmanuel (Kongwa).

Wengine ni Jabir Shekimweri (Dodoma), Gift Msuya (Chamwino), Said Nkumba (Bukombe), Peres Magiri (Kilolo), Kanali Wilson Sakullo (Misenyi), Kanali Mathias Kahabi (Ngara) na Jamila Kimaro (Mpanda).

Pia yupo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, Kanali Michaeli Ngayalina (Buhigwe), Kamali Evance Mallasa (Kakonko), Kanali Aggrey Magwaza (Kibondo),Kanali IssackMwakisu (Kasulu), Kanali Hamis Maiga (Rombo), Abdallah Mwaipaya (Mwanga) na Shaibu Ndemanga (Lindi).