Rais Samia ateua Mwenyekiti Tira

Muktasari:

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Moremi Marwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (Tira).

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Moremi Marwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus imesema uteuzi huo umeanza Mei 14, 2023.

Marwa ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) pia aliwahi kuhudumu kwa miaka tisa kama Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Mamlaka ya (Tira) ilianzishwa chini ya Sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 yenye jukumu la kuratibu sera na mambo mengine yanayohusu bima katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.