Rais Samia ateua wawili, yumo bosi wa Veta
Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) na Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) na Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati.
Ambapo amteua Anthony Kasore kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Kabla ya uteuzi huo, Kasore alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Aidha, Rais Samia amemteua Goodluck Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo, Shirima alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria na uhusiano wa kampuni ya Puma.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Ijumaa Aprili 12, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.