Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 5,704

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,704 katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara leo Desemba 27

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,704 katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru.


Akizungumza na wandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 27, 2021 Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema Rais Samia ametoa msamaha huo kwa masharti ikiwa ni pamoja na wafungwa hao wawe wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia kabla ya Oktoba 9, 2021.