Rais Samia awataka viongozi kujitathmini

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika mwendelezo wa ziara yake katika mkoani Lindi.
What you need to know:
- Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na mgawo wa fedha za maendeleo zinazotolewa wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi wilaya hiyo isipobadilika viongozi wakae wajitazame.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na mtiririko wa fedha zinazopelekwa na Serikali wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, wilaya hiyo isipobadilika viongozi wajitazame.
Ameyasema hayo leo Septemba 19, 2023 akiwa wilayani humo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara aliyoianza Septemba 16, 2023.
Amesema awali wakati Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge akitaja fedha walizopokea kutekeleza miradi ya maendeleo, hakutaja fedha za elimu.
“Mbunge aliyesimama, amezungumzia umeme, maji na barabara, hakuzungumzia elimu, huko nako Serikali inamimina fedha nyingi sana. Sasa ndugu zangu wa Kilwa, kwa mtiririko huu wa fedha, Kilwa isipobadilika naomba mjitazame kuna nini.
Huku akibainisha kuwa na taarifa za utedaji wa madiwani, wenyeviti wa halmashauri katika utendaji wa miradi hiyo, amewataka watendaji hao kuhakikisha fedha hizo zinawanufaisha wananchi.
“Niwaambie kwamba hizi fedha zinaletwa kwa aajili ya kuondoa fedha zikatatue changamoto ana adha kwa wananchi. Ndiyo maana nasema mtiririko huu wa fedha, Kilwa isipobadilika viongozi kaeni mjitazame kuna nini ndani yenu.
Mbunge Kasinge amemshukuru Rais Samia kwa fedha zinazotolewa na Serikali ukiwamo ujenzi wa bandari ya uvuvi.
Hata hivyo, ametaka changamoto za wananchi kuwa pamoja na migogoro ya ardhi, akitaja eneo la mradi wa bandari, akisema baadhi ya wananchi hawajalipwa fidia.
“Ulipomteua rafiki yangu Waziri Jery Silaa nikamwambia kazi ya kwanza ni kwenda kushughulika na migogoro hii,” amesema.
Pia alitaja suala la kutolipwa fidia kwa wananchi 438 waliopisha ujenzi wa uwanja wa ndege wilayani humo, huku akigusia migogoro ya wakulima na wafugaji katika kata za Kiranjeranje, Likawage na Kikole na kero ya wanyama waharibifu.