Rais Samia kuongoza kamati kuu CCM, wagombea Eala kupatikana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan
What you need to know:
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakutana leo Jumatano, pamoja na mambo mengine kitajadilia na kuteua wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano, Septemba 7, 2022 anaongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.
Katika kikao hicho kinafanyikia Ofisi ndogo za chama, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kujadili masuala mbalimbali, kitajadili na kupitia majina ya wanachama walioomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala)
Tayari mchujo wa wagombea ulifanyika Septemba 4 na 5, 2022 makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.
Jana Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa ya uchaguzi huo wa wajumbe tisa utakaofanyika Septemba 22, 2022 saa 5:00 asubuhi, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.
Hadi sasa vyama vya ACT-Wazalendo na CUF wameshakamilisha mchakato wa kupata majina ya watakaoenda kupigiwa kura Bungeni huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kutoshiriki.