Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia mgeni rasmi siku ya mashujaa

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kabla ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha Julai 17, 2023.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan licha ya kuwa mgeni rasmi kesho katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa, ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa uwanja mpya unaojengwa Mtumba jijini Dodoma.

Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatakayofanyika katika uwanja mpya uliopo Mtumba jijini Dodoma.

 Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano kwa umma cha wizara hiyo leo Jumatatu Julai 24, 2023.

“Shughuli za maadhimisho hayo ni pamoja na gwaride la maombolezo, uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye mnara wa mashujaa pamoja na dua/sala kutoka kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini,”amesema Mhagama.

Pia amesema Rais ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja mpya wa kumbukumbu za mashujaa.

Amesema katika kukuza uzalendo kwa wananchi, maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa na wilaya zote hapa nchini kwa kufanya shughuli za kijamii kama vile kupanda miti.

Shughuli nyingine ni kufanya usafi maeneo ya kijamii na kufanya kumbukumbu ya mashujaa kwa mikoa na wilaya ambayo ina minara au makaburi ya mashujaa.

Mhagama amewahamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma kufika mapema kuanzia Saa 12 asubuhi kesho kwenye kumbukumbu hizo muhimu kwa historia ya nchi.

Pia amewataka kuendelea kuwa wazalendo na kutunza tunu za nchi za amani na utulivu.