Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Samia awasili na magwanda ya jeshi miaka 60 JKT

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amevalia gwanda za jeshi. Picha na Mtandao

Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma na kukagua gwaride la maadhimisho ya miaka 60 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 Rais amewasili saa 4.04 asubuhi akiwa amevaa vazi la Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amepanda jukwaani kupokea heshima ya utii na wimbo wa Taifa.

Kilele cha maadhimisho hayo kinafanyika leo Jumatatu Julai 10, 2023 sambamba na uzinduzi wa kitabu cha miaka 60 ya JKT.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jacob Mkunda, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Jumaa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk Eliezer Feleshi.

JKT ilianzishwa Julai 10, 1963, katika kuelekea siku ya maadhimisho hayo walikuwa na maonyesho mbalimbali Jiji Dodoma, sehemu kubwa wakionyesha bidhaa zinazozalishwa na JKT.