Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Shein kuzindua mpango wa kutokomeza malaria

Muktasari:

ais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein atazindua mpango maalum wa kutokomeza kipindupindu visiwani humo ambao utahusisha taasisRais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Septemba 10, 2019 atazindua mpango maalum wa miaka kumi wa kutokomeza kipindupindu visiwani humo.i mbalimbali za Serikali

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Septemba 10, 2019 atazindua mpango maalum wa miaka kumi wa kutokomeza kipindupindu visiwani humo.

Wazir wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed alibainisha hayo leo Septemba 6, 2019 amesema mpango huo ambao utazijumuisha taasisi saba una lengo la kuhakikisha Zanzibar hakuna kipindundi kama ilivyofanikiwa kuondoa maradhi ya Malaria kwa kufikia asilimia 0.4.

Miongoni mwa taasisi ambazo zinashiriki katika mpango huo ni Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya nchi Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Wizara ya ujenzi, mawasiliano na usafirishaji.

“Mbali ya taasisi hizo lakini pia tutakuwa na washirika wa maendeleo ambao ndio wanaotuunga mkono katika mpango wetu huu wakiwemo WHO, UNICEF, KOICA pamoja na mashirika mengine mbalimbali ambao wao watatusaidia kifedha pamoja na kutoa elimu juu ya kukabiliana na maradhi hayo,” alisema

Waziri Mohamed amesema katika kufanikisha mpango huo, tayari serikali imejipanga vyema kwa kuandaa sheria maalum za kinga dhidi ya maradhi, Sheria ya kukabiliana na majanga, kuboresha miundombinu ya maji safi na salama.

Pia,  kuimarisha mitaro ya kupitishia maji taka ili kuzuia kutwama ovyo takataka na maji machafu mitaani pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya mbali mbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji kamisheni maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame alisema katika kuhakikisha mpango huo alisema kukamilika kwa mradi mkubwa wa kupitisha mitaro ya maji taka katika Mkoa wa mjini Unguja ni hatua moja ya kufikia malengo ya kutokomeza maradhi ya kipindu pindu hasa katika maeneo ya mjini.