Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa mahakama ya Afrika kufanya ziara Mauritania

Watu saba wafikishwa kortini wakidaiwa kujipatia Sh 428milioni mali ya Tanesco

Muktasari:

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR), Jaji Iman Daud Aboud pamoja na viongozi wengine wa mahakama hiyo watafanya ziara ya siku tatu nchini Mauritania.

Arusha. Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR), Jaji Iman Daud Aboud pamoja na viongozi wengine wa mahakama hiyo watafanya ziara ya siku tatu nchini Mauritania.

Ziara hiyo itaanza Agosti 15 hadi 17 mwaka huu ambapo lengo la ziara hiyo ni kuhimiza nchi ya Mauritania kutoa tamko ili kuruhusu watu binafsi kuifikia mahakama hiyo moja kwa moja.

Mauritania iliidhinisha itifaki ya mkataba wa Afrika wa haki za kibinadamu na watu kuhusu kuanzishwa kwa mahakama hiyo Desemba 14, 2005 ambapo mpaka sasa haijatoa tamko chini ya kifungu cha 34(6) B.

Akizungumzia kuhusu ziara hiyo, Rais huyo amesema mafanikio ya mahakama kama utaratibu uliowekwa wa kulinda haki za binadamu yanahitaji uidhinishaji mpana wa itifaki kwa nchi wanachama pamoja na kuikubali mahakama kwa kutoa tamko chini ya ibada ya 34(6).

"Uidhinishaji huu wa jumla utaipa mahakama uhalali unaohitaji ili kutekeleza wajibu wake ipasavyo,"amesema

Jaji Imani amesema nchi ambazo zimeweka tamko hilo mpaka sasa ni nchi ya Burkina Faso, Gambia, Ghana, Guinea Bissau, Malawi, Mali, Niger na Tunisia.

Ameongeza "Ziara hii pia ni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu barani Afrika, kuongeza uelewa kuhusu mahakama, kuhimiza uidhinishaji wa itifaki na kutoa tamko linaloruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuleta mashauri moja kwa moja mahakamani,"

"Pamoja na kuhimiza umma kutumia mahakama katika kutatua migogoro ya haki za binadamu na kuhimiza matumizi ya mahakama kwa maoni ya ushauri,"

Mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha inaundwa na majaji 11, raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika waliochaguliwa kwa nafasi zao binafsi.