Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Namibia kufanya ziara ya kitaifa Tanzania

Rais wa Namibia, Dk Netumbo Nandi-Ndaitwah.

Muktasari:

  • Rais huyo wa Namibia alifanya ziara yake kwa mara ya kwanza nchini Mei, 2025 kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dar es Salaam. Rais wa Namibia, Dk Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kesho Ijumaa, Juni 19, 2026, kwa ziara ya kitaifa yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Ziara hiyo itakuwa ya pili kwa Rais Nandi-Ndaitwah kutembelea Tanzania tangu alipoingia madarakani Desemba 2024 hatua inayotajwa kuendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu uliojengwa kwenye misingi ya harakati za ukombozi wa Afrika, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu leo Juni 18,2026,  Rais huyo wa Namibia anatarajiwa kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumamosi Juni 20, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Mazungumzo hayo yanatarajiwa kujikita katika masuala ya ushirikiano wa nchi mbili, pamoja na changamoto na fursa za kikanda na kimataifa zinazohusu maslahi ya pamoja ya Tanzania na Namibia," amesema Machumu.

Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Katika ziara hiyo, Rais Nandi-Ndaitwah atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambako aliwahi kuishi miaka ya 1980 alipokuwa Mwakilishi Mkuu wa Chama cha South West Africa People's Organization (Swapo).

Eneo hilo lina umuhimu wa kihistoria kutokana na nafasi ya Tanzania kusaidia harakati za ukombozi wa Namibia na nchi nyingine za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha, Rais huyo ambaye atahitimisha ziara yake nchini Juni 22, 2026 na kabla ya kuondoka atatembelea kambi ya wapigania uhuru wa harakati za ukombozi Afrika iliyopo Kongwa, mkoani Dodoma, eneo linalohifadhi historia ya mchango wa Tanzania katika ukombozi wa bara hilo.