Ras Songwe agoma kukagua mradi bila nyaraka

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda.
Muktasari:
- Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, amewajia juu watendaji katika Halmashauri ya Mji Tunduma, baada ya katika eneo la miradi bila na hivyo kusababisha ukaguzi kukwama.
Tunduma. Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, amewajia juu watendaji katika Halmashauri ya Mji Tunduma, baada ya katika eneo la miradi bila na hivyo kusababisha ukaguzi kukwama.
Hali hiyo imejitokeza wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, iliyotengewa fedha kutoka Serikali Kuu na ile ya fedha za mapato ya ndani katika halmashauri hiyo.
"...wanaohusika katika kusimamia miradi ya maendeleo hakikisheni mnatunza nyaraka na vielelezo vyote vya miradi inayotekelezwa kwa fedha za umma," amesema Seneda.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika Shule ya Machinjio, iliyopo Mtaa wa Machinjio katika halmashauri hiyo, unaogharimu Sh105 milioni, Seneda alishindwa ameshindwa kufanya ukaguzi baada ya kukosekana nyaraka muhimu za mradi huo.
“Kwa Tunduma tatizo hili linajirudia kila mara wakati tukija kukagua miradi tunalikuta, wataalamu hakikisheni mnatunza vizuri nyaraka zote za miradi...sasa hapa nimeomba ramani ili nianze kukagua maana kama huna ramani huwezi kufanya ukaguzi wowote kwa kuwa huwezi kujua makisio ya gharama za mradi, lakini naambiwa haipo" amesema Seneda kisha kuondoka eneo la mradi bila kulikagua.
Mradi huo wa nyumba mbili unagharimu kiasi cha Sh105 milioni ambapo Serikali Kuu imetoa kiasi cha Sh55 milioni, huku halmashuri kupitia mapato ya ndani ikiwa imetoa kiasi cha Sh50 milioni.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Alex Msuya, ambaye ni Kaimu Ofisa Mipango alimueleza Katibu Tawala huyo kuwa nyaraka za mradi huo zilichukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana ma Rushwa (Takukuru) na hazijarejeshwa.
Mradi wa pili alioutembelea Katibu Tawala Seneda ni wa ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Sogea ambapo licha kufanya ukaguzi hakufanikiwa kupata baadhi ya nyaraka za utekelezaji wa mradi huo, kitendo ambacho kilimlazimu kuagiza kupatiwa nyaraka zote kabla ya kumaliza ziara katika halmashauri hiyo.
Mradi zahanati ambao hadi wakati wa ziara, ujenzi wake umefikia asilimia zaidi ya 90 huku zikiwa zimetumika zaidi Sh180 milioni pamoja na nguvu za wananchi zenye dhamana ya Sh12 milioni.
Msimamizi wa mradi huo, Aizack Sinienga, ambaye ndiye Mtendaji wa Kata ya Sogea amesema mradi huo wa Zahanati unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba baada ya Serikali kutoa kiasi kingine cha Sh10 milioni, zilizoombwa kwa ajili ya kukamilisha shughuli zilizobaki na Zahanati kuanza kutoa huduma.
Hii ni ziara inayohusisha wataalam wa sekretarieti ya mkoa wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa ambao wameanza ziara ya kutembelea halmashauri zote tano za mkoa huu ikiwa ni hatua ya kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo kutoa maelekezo na ushauri.