Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC ataja mafanikio ya sensa Kilimanjaro

Muktasari:

  • Mkoa wa Kilimanjaro tayari umehesabu kaya 441,000 sawa na asilimia 101.5, katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 23, mwaka huu.

  


Moshi. Mkoa wa Kilimanjaro tayari umehesabu kaya 441,000 sawa na asilimia 101.5, katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 23, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Agosti 30, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa wakuu waandamizi wa makao makuu ya polisi na makamanda wa polisi wa mikoa kinachofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro.

Babu amesema kazi ya Sensa imefanyika vizuri na katika siku zilizoongezwa, watahakikisha wale ambao walikuwa hawajafikiwa, wanahesabiwa na Sensa ya majengo inafanyika kwa ufanisi.

"Sensa Kilimanjaro imefanyika vizuri, watu 441,000 wamehesabiwa sawa na asilimia 101.5 na kazi inaendelea, tutahakikisha watu wote wanafikiwa," amesema Babu.

Akizungumzia kuhusu chanjo ya Uviko, Babu amesema katika mkoa huo watu waliochanja hadi Agosti 28 mwaka huu ni 942,000 sawa na asilimia 75.6 ya lengo lililokusudiwa.



Aidha babu anemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miradi ya maendeleo inayotekekezwa katika Mkoa huo ambapo amesema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2022/2023, Mkoa umetengewa Sh 350 bilioni na kati ya hizo Sh78 bilioni ni za miradi ya maendeleo.