Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Babu awapa maagizo wakuu wa wilaya Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewaagiza wakuu wa wilaya zinazopakana na nchi jirani za mkoa huo kuhakikisha wanachukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola ambao umeutikisa nchi jirani ya Uganda.


Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewaagiza wakuu wa wilaya zinazopakana na nchi jirani za mkoa huo kuhakikisha wanachukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola ambao umeutikisa nchi jirani ya Uganda.

Wilaya ambazo zinapakana na nchi jirani katika mkoa wa Kilimanjaro ni Wilaya ya Rombo ambayo ina mipaka miwili mikubwa ya Tarakea na Holili, Siha, Pamoja na wilaya ya Mwanga.

Babu ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi pamoja na wakuu mbalimbali wa idara katika kikao kazi cha kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa mpango wa Tasaf kipindi cha pili katika mkoa huo.

Amesema ugonjwa huo ni hatari na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya ugonjwa huo na kusema tayari wizara ya afya imeshatoa maelekezo ya namna ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo katika maeneo ya mipakani.

"Tujihadhari sana na ugonjwa huu wa Ebola, ugonjwa huu ni hatari na haukwepeki, Wizara ya afya kupitia Waziri Ummy Mwalimu imetoa maelekezo hasa katika maeneo yaliyopo mpakani kama Rombo, Siha, Mwanga na maeneo yote yaliyopo mkoa wa Kilimanjaro,"

"Naomba ndugu zangu wakuu wa Wilaya tuwaambie wananchi wetu wachukue tahadhari kabisa juu ya ugonjwa huu wa Ebola, "amesema RC Babu