Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Babu awataka wenye ‘guest’ kuorodhesha wageni

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Agosti 22 kuhusu maandalizi ya sensa mkoani humo ambapo amesema yamefikia asilimia 96. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema maandalizi ya sensa mkoani humo yamekamilika kwa asilimia 96, huku akiwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni na kambi za watalii kutoa ushirikiano.

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wamiliki wa kambi za watalii pamoja na nyumba za kulala wageni mkoani humo, kujaza fomu maalum ambayo imepelekwa kwa kila nyumba za kulala wageni zitakazoonyesha wageni waliolala usiku wa kuamkia Agosti 23 katika maeneo hayo.

Babu ametoa agizo hilo leo Agosti 22, wakati akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi katika mkoa huo, akisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 96.

“Napenda kutoa wito kwa wamiliki wote wa hoteli, lodge, guest na kambi za watalii kutoa ushirikiano wa kuhakikisha kuwa wateja wote watakaolala katika nyumba hizo usiku wa Agosti 22 kuamkia Agosti 23 wanajaza fomu maalum ambayo imepelekwa kwa kila nyumba ya kulala wageni,” amesema RC Babu.

Aidha amewataka watendaji wote wa kata, vijiji, wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa yote ndani ya mkoa huo kutoa hamasa kwa wananchi wa maeneo yao na ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa watakapokuwa katika maeneo yao ya kiutawala.

“Nina waagiza wakuu wote wa wilaya kufuatilia mwenendo wa zoezi zima la sensa ya watu na makazi katika wilaya zao ikiwa ni pamoja na usalama wa makarani na vitendea kazi vyao,” amesema.

Amesema matokeo ya takwimu za sesa ya mwaka 2022 yataiwezesha Serikali kupima kiwango cha maendeleo kulichofikiwa na kupanga mipango ya maendeleo kwa wakati ujao na kwamba takwimu zinazotokana na sensa huwezesha kutoa huduma ya maji, afya, elimu, kwa kuzingatia Idadi ya watu.




Amesema kazi hiyo itaendelea kwa takribani siku sita au saba na baada ya hapo itafuata sensa ya majengo itakayofanyika kwa muda wa siku tatu.

"Hivyo unachotakiwa kukifanya ni kuorodhesha na kuandika kwenye karatasi taarifa ya watu wote watakaoalala kwenye kaya husika usiku wa kuamkia Agosti 23 ili karani atakapofika kwenye kaya hiyo mkuu wa kaya au mwanakaya atakayekuwepo aweze kutoa taarifa hizo,” amesema RC Babu