Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Kagaigai avitaka vyombo vya usalama Kilimanjaro kusimamia haki ya mtoto

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameviagiza vyombo vya usalama mkoani humo kuhakikisha vinasimamia haki katika utekelezaji wa sheria dhidi ya vitendo vya ukatili.

  




Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameviagiza vyombo vya usalama mkoani humo kuhakikisha vinasimamia haki katika utekelezaji wa sheria dhidi ya vitendo vya ukatili.

Kagaigai ameyasema hayo leo Jumatano Juni 15, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, yanyofanyika Juni 16 kila mwaka.

Amesema maadhimisho hayo kimkoa yatafanyika kwa njia ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto, amewataka wadau wa watoto kusimamia utoaji na upatikanaji wa haki za watoto.

"Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kisheria na kiutawala kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa maendeleo ya mtoto yanakuzwa ,kulindwa na kuendelezwa kuanzia ngazi ya familia ,jamii na Taifa.

"Navitaka vyombo vya dola katika mkoa wetu kuhakikisha vinasimamia vyema na kwa haki utekelezaji wa sheria zinazohusu masuala ya watoto yakiwemo umahiri katika kushughulikia mashauri ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto yanayotolewa taarifa,"amesema

Aidha amewataka viongozi wa dini na wa kimila mkoani humo kuendelea kuhimiza waumini na washirika wao juu ya maadili mema na kuwa na hofu ya Mungu katika kutembea katika misingi mikuu ya imani zao.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema"Tuimarishe ulinzi wa mtoto ,tokomeza ukatili dhidi yake,jiandae kuhesabiwa,".Kilimanjaro bila vitendo vya ukatili dhidi ya watoto inawezekana,tushirikiane sote kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika 16 Juni kila mwaka