RC Kigaigai: Anayetafuta utajiri kupitia uaskari hatufai
Muktasari:
- Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amewataka vijana waliopeleka maombi ya kutaka kujiunga na Jeshi la Magereza mkoani humo kuhakikisha wanakuwa wazalendo na kulitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa pindi watakapochaguliwa.
Moshi. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amewataka vijana waliopeleka maombi ya kutaka kujiunga na Jeshi la Magereza mkoani humo kuhakikisha wanakuwa wazalendo na kulitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa pindi watakapochaguliwa.
Kagaigai ameyasema hayo leo Juni 27, 2022 wakati akizungumza na vijana hao wapatao takribani 66.
"Wale watakaochaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza, tutafurahi kupata vijana ambao wana mapenzi na nchi yao kwasababu kazi ya uaskari ni kazi ambayo inahitaji kujituma, kujitoa, kuwa na uadilifu na uaminifu na mapenzi makubwa na nchi," amesema Kigaigai.
"Nawatakia kila la kheri lakini muende mkijua kwamba kazi ya uaskari sio kazi ya kutafuta utajiri ni kazi ya kulitumikia Taifa na kujitoa," amesema Kagaigai.
"Kwa maana hiyo nawashauri kwa yeyote atakayesema anatafuta utajiri kwa kupitia uaskari akafanye biashara kwani kazi ya uaskari ni kulitumikia Taifa kwa uzalendo ,uadilifu na uaminifu," amesema Kagaigai.
Tayari vijana hao wameshafanyiwa usaili kwa ngazi ya wilaya na sasa wapo ngazi ya mkoa.