Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Kilimanjaro awapa agizo DC, DED Hai

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai akiwa pamoja na kamati ya usalama ya Mkoa huo wakikagua ujenzi wa shule mpya inayojengwa katika kijiji cha Shirimatunda,Kata ya Mnadani wilayani Hai.picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC), Juma Irando na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo (DED) kuhakikisha ujenzi wa mradi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa Kijiji cha Shirimatunda, kata ya Mnadani Wilayani humo inakamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Stephen Kagaigai amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Irando na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha ujenzi wa mradi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Shirimatunda inakamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, amesema kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo ambayo Serikali imetoe Sh600 milioni itaondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu pamoja na kuwapunguzia wazazi gharama za nauli za kila siku.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi hakikisheni ifikapo Juni 30 mwaka huu shule hii iwe imekamilika, naomba spidi ya ujenzi huu iongezeke ili wananchi wa kijiji hiki waweze kupata manufaa ya shule hii inavyotakiwa," amesema na kuongeza

"Ujenzi wa shule hii mpya katika Kata hii ya Mnadani ni maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, ameona watoto wetu wasitembee umbali mrefu wapate huduma hii ya elimu karibu, hivyo kwa moyo wa dhati kabisa ameona ni vyema wananchi wake wapate huduma nzuri ili tuweze kusonga mbele kimaendeleo,"amesema Kagaigai

Baadhi ya wananchi wa Kata hiyo, wameipongeza Serikali kwa uwepo wa ujenzi wa shule hiyo na kusema kwa muda mrefu watoto wao wamekuwa wakitaabika wakitembea zaidi ya kilomita 17.

Mkazi wa Kata ya Mnadani, Cornel Mushi amesema wamefarijika sana kuona namna Serikali inavyowapigania kwani watoto wao kutokana na umbali wa shule wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali za barabarani ikiwemo kubakwa na wengine kurubuniwa na kuacha shuule.

"Tumefarijika sana kujengewa shule hii ya sekondari na Serikali kwa sababu watoto wetu walikuwa wakitembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 17 kwenda shule na njiani kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo wanafunzi kubakwa na wengine kuacha shule kutokana na changamoto ya umbali,"

"Uwepo wa shule hii itatusaidia sana sisi wazazi pamoja na watoto wetu maana tutakuwa tumepunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu, wakati mwingine kutokana na mwanafunzi kutembea umbali mrefu, akiingia darasani tayari ameshachoka na hata kumwelewa mwalimu darasani ni changamoto,"

Mkazi wa kijiji cha Shirimatunda, Germana Mallya amesema uwepo wa shule hiyo ni neema kwa wazazi na kuishukuru Serikali kwa kuwa sikivu na kuwasogezea huduma muhimu za shule kwenye maeneo ya karibu.

"Tunahesabu ni neema kupata shule hii, tunaamini shule hii itakuwa ni ukombozi kwa watoto wetu kwani watasoma karibu na wazazi angalau tutajisikia watoto wetu kuwa wako salama,"