Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Manyara aongoza upandaji miti 133,000 Ziwa Bassotu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Kampeni ya siku saba ya upandaji miti ziwa Bassotu Wilayani Hanang' Mkoani Manyara imelenga kutunza mazingira ili kunusuru kina chake kupungua kutokana na kukaa matope

Hanang'. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amezindua kampeni ya nitunze nikutunze kwa kuongoza upandaji miti 133,000 kuzunguka Ziwa Bassotu wilayani Hanang'.

 Pia, Makongoro ameziagiza Hospitali ya Rufaa ya Haydom yenye shamba Mulbadaw na kampuni ya Ngano Ltd, kushughulikia makorongo yanayobeba udongo na taka kutoka kwenye mashamba ya ngano.

"Na ninyi mnaoishi karibu na kulizunguka ziwa Bassotu hakikisheni miti hii 133,000 mnaitunza ili kauli mbiu ya nitunze nikutunze iwe na faida kwa kizazi cha sasa na cha baadaye," amesema Makongoro.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang', Janeth Mayanja amesema ziwa Bassotu lina changamoto ya kina cha maji kupungua kutokana na kujaa tope zinazotokana na ongezeko la shughuli za kibinadamu.

"Shughuli hizo ni kama kilimo, ukataji miti na uoto wa asili kuzunguka ziwa Bassotu hivyo kwa kushirikiana na wadau tukafanikisha upatikanaji wa miti hiyo," amesema Mayanja.

Mvuvi wa ziwa Bassotu, John Tluway amesema kwa sababu wanategemea maisha yao ya kiuchumi kwa kuvua samaki wanaungana na serikali kutunza miti hiyo.