RC Pwani atatua kero za maji papo hapo

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge (mbele katikati ) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji ya bomba Kijiji cha Mjawa Kibiti alipokua kwenye ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Kibiti.

Muktasari:

  • Utatuzi kero ya maji iende sambamba na wananchi kutumia maji safi na salama kwa uangalifu, walinde miundombinu pia wachangie bili ndogo za maji ili huduma iiwe endelevu kwenye meneo yao.

Kibiti. Adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili wakazi zaidi ya 13,000 wanaoishi Bungu wilayani Kibiti mkoani Pwani inakwenda kukoma baada ya ujenzi wa miradi miwili ya maji ya bomba kufikia asilimia 85 katika kijiji cha Jaribu Mpakani.

Kukamilika kwa miradi hiyo miwili yenye thamani ya Sh1.4 bilioni pia itaweza kuchangia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama mkoani Pwani ambacho kwasasa upatikanaji wake ni asilimia 86.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema hayo leo Novemba 7 alipokua  kwenye ziara ya ukaguzi wa utekelezaji miradi ya maendeleo sambamba na  kusikiliza  kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa papo na zingine kuzichukua kwenda kutafutia majawabu.

Akiwa Kibiti, Kunenge ameanza ziara kwa kukagua miradi miwili ya maji ya bomba katika kijiji cha Jaribu Mpakani  na kijiji cha Mjawa yenye thamani ya Sh1.3 bilioni na yote inatekelezwa na Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini (Ruwasa).

Miradi hiyo ambayo ujenzi wake ipo katika hatua za mwisho kukamilika inata-rajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 13,400 wa vijiji hivyo ambao kwa sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu mpaka kilometa nne kufuata maji kwenye vyanzo visivyo rasmi na salama kwao.

Amewaagiza kandarasi wanaojenga miradi hiyo M/S Trinity Manuctures Ser-vice ltd wanaojenga mradi wa maji Kijiji Cha Mjawa  na M/S Broadway Engi-neering Co.Ltd wanaojenga Jaribu Mpakani kuhakikisha wanafanya kazi us-iku na mchana ili kukamilisha mapema na wananchi waanze kupata maji safi na salama na kwa gharama iliyonafuu.

"Mhandisi nimesema uzingatie utaalamu kama ni siku 21 wewe ni mtaalamu pale ambapo hapaitaji  siku 21 fanya kazi usiku na mchana tuweze kumaliza kazi mapema na umeniambia kazi nyingi zimekamilika, tumeweka lengo Aprili iwe tayari lakini tukimaliza mapema zaidi itakuwa faraja kwetu kwasababu wananchi hawa watapata maji safi na salama mapema," amesema Kunenge

Kunenge amewataka wananchi wa Halmashauri ya Kibiti  kuendelea kutumia maji kwa uangalifu na kulinda miundombinu ya maji sambamba na  kuchan-gia gharama kidogo (bili za maji) kwa ajili ya uendeshaji wa miradi ya maji iliyopo kwenye maeneo yao.

Awali kaimu Meneja wa Ruwasa Kibiti, Juma Ndaro amesema kazi zilizobakia kwenye miradi hiyo miwili ni pamoja na ufungaji wa pampu ya kusukumia maji, kuunganisha umeme katika nyumba ya mitambo kwa ajili ya kusukumia maji, ujenzi wa ofisi ya watumia maji na nyumba ya watumishi wa bodi na ufungaji pampu ya kusukumia maji yenye uwezo wa kutoa lita 17,000 kwa saa.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho wameshukuru Serikali kwa kuwainua wananchi kiuchumi na kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya maji safi na salama.

"Sisi kina mama huu mradi utakua mkombozi kwetu maana tumechoka kutembea mbali kilometa nne kusaka maji, na wakati mwingine tunapata ya-siyo salama lakini tunabeba maana hata hayo salama hayapo, kwahiyo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kibiti na sisi tunaanza kupata maji safi na salama," amesema Magreth.

Katika ukaguzi miradi vya Elimu, Kunenge alipokua kwenye shule ya Sekondari Jaribu iliyojengwa kupitia mradi wa kuboresha elimu Sekondari (SE-QUIP) amesema suala la kujengwa eneo hilo ni muhimu sababu limepunguza umbali kwa wanafunzi wa Kijiji cha Mjawa kutembea zaidi ya kilometa tano kwenda Kijiji cha jaribu Mpakani

Amesema ujenzi katika eneo hilo bado linaendelea kwani ipo asilimia 80 na ni kutokana na eneo hilo linahitaji fedha nyingi zaidi kwa sababu lipo eneo la mteremko sio tambarare.

"Tupo na Katibu Tawala mkoa, Rashid Mchatta tutasaidia kufatilia maombi ya fedha Tamisemi tupate fedha zaidi za kukamilisha ujenzi, pamoja na majengo kukamilika lakini landscaping eneo lenyewe liweze kutengezwa vizuri ili rahisi kwa watoto kuweza kuja katika madara,”