Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ridhiwani: Waratibu wa Tasaf tendeni haki

Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya watumishi wa Tasaf.

Muktasari:

  • Kutokana na malalamiko ya baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania (Tasaf), waratibu wa mpango huo wamekumbushwa kutenda haki.

Iringa. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini (Tasaf), kuwatenda haki kwa wanufaika wa mpango huo.

Akizungumza na watumishi wa umma katika ziara yake mkoani Iringa leo Novemba 21, Kikwete amesema waratibu hao wanapaswa kuwajibika katika kutatua kero za wanufaika wa mfuko huo na kutenda haki.

"Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeweka lengo la  kuhakikisha inawanusuru wananchi katika wimbi la umasikini, imeongeza fedha kwa walengwa, tendeni haki ili fedha hizi ziwasaidie kujikwamua kiuchumi," amesema Ridhiwani.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema yapo baadhi ya malalamiko kutoka kwa walengwa ikiwemo kuondolewa kwenye mpango huo.

Amesema mpango wa Tasaf uliopo sasa utakwenda mpaka mwaka 2025 kabla ya kuandaliwa mwingine, hivyo walengwa waliopo wanapaswa kuendelea kuwepo.

Amesema suala la vigezo kwa wanufaika vinatakiwa vizingatiwe ili kuepuka kuwanufaisha wasiostahili.

Naye Mkurugenzi wa Tasaf, Shadrak Mziray amepiga marufuku mtindo wa kuwatumia wazee wanufaika wa mpango huo kufanya kazi kwenye miradi inayotekelezwa na walengwa.

Amesema ikiwa mzee huyo katika familia yake hakuna mtu anayeweza kufanya kazi kwenye miradi hiyo, basi anapaswa kupewa pesa zake huku jambo la muhimu likiwa mahudhurio.

Amesema Tasaf imefanikiwa kuhudumia kaya masikilini milioni 1.3, huku Iringa kukiwa na kaya 30,000.