Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia kuzindua ukarabati madarasa ya Tasaf Kizimkazi

Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Shadrack Mziraya aliyevaa koti akiwa na viongozi mbalimbali wa Zanzibar wakikagua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mfuko huo.

Muktasari:

  • Ukarabati na ujenzi wa shule ya sekondari na msingi ya Kizimkazi, uliotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), sasa umekamilika kuzinduliwa keshokutwa na Rais Samia Samia Suluhu Hassan.

Unguja. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua shule za sekondari ya msingi na Kizimkazi zilizopo Mkoa wa Kusini Unguja zilizokarabatiwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika Jumanne Agosti 29, 2023 mjini Unguja, uzinduzi huo ni sehemu ya shamrashamra ya Tamasha la sherehe za Kizimkazi.

Tamasha hilo lilianzishwa rasmi Agosti mwaka 2015 likitambulika kwa jina la Samia day kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2018 na kuitwa Kizimkazi Day lengo likiwa ni kutangaza utamaduni, vivutio na rasilimali za Kizimkazi mbapo hufanyika Agosti ya kila mwaka.

Ukarabati huo umekwenda sambamba na uboreshaji wa ofisi za walimu na maabara, matundu ya vyoo 14, ukumbi wa mikutano shughuli iliyogharimu Sh 277 milioni.

Akizungumza jana Jumamosi Agosti 26, 2023 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk Islam Seif Salum amesema shughuli ya ujenzi wa shule umemalizika na kilichobaki ni kuweka madawati, meza na viti, huku akiwapongeza mafundi kwa kutekeleza vema majukumu yao.

“Tunasubiri kwa hamu Kizimkazi tuonyeshe maendeleo yetu hii Tasaf pamoja na kusaidia kaya maskini lakini pia inajishughlika na uboreshaji wa miundombinu ya shule na hospitali,”amesema Dk Salum.

Kaimu mkurugenzi wa Tasaf, Shadrack Mziray amesema  taasisi inatekeleza majukumu yake bara na visiwani, akisema kumekuwa na maendeleo ya ukarabati wa shule ya Kizimkazi. Amesema shughuli hiyo ilitakiwa ichukue mwaka mmoja, lakini mafundi wameifanya kwa miezi sita.

“Ukizungumzia Tasaf watu wanajua inafanya jambo moja la kuziwezesha kaya maskini kwa kuzipa ruzuku, bali tunatekeleza majukumu pia ya kutoa ajira za muda sambamba na kuboresha miundombinu,”amesema Mziray.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Siajabu Suleiman Pandu amesema kumekuwa na utofauti mkubwa wa mwonekano wa shule ya Kizimkazi baada ya kufanyiwa maboresho makubwa ya miundombinu.

“Tunaishukuru Tasaf wametoa fedha kwa wakati kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hii, kilichobaki ni taratibu ndogo ndogo ikiwemo usafi kabla ya mwenye jambo lake (Rais Samia) kuja kutembelea.Wananchi wawe watulivu na kumsubiri mama yetu (Rais Samia) ambaye atakuwa sehemu ya baraka ya tukio hili,” amesema Pandu.