Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rufiji wapata huduma ya X Ray kwa mara ya kwanza

Rufiji. Kilio cha muda mrefu cha kukosa huduma ya x-ray kwa wakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kimeisha baada ya  kujengwa jengo la kutoa huduma hiyo.

Jengo hilo limejengwa na halmashauri hiyo kwa Sh139 milioni.

Akizungumza na Mwananchi Digital jana  Jumamosi Januari 14, 2022 mkurugenzi wa halmashauri hiyo, John Kayombo amesema kukamilika kwa huduma hiyo kutapunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kwa wakazi wa eneo hilo kufuata huduma ya x-ray wilaya jirani.

“Tunamshukuru Rais Samia baada ya sisi kukamilisha jengo na miundombinu muhimu kwa muda wa miezi sita tu, ametuletea x-ray mpya ya kidijitali na sasa wananchi hawaendi tena hospitali ya Mchukwi iliyopo wilaya ya Kibiti kufuata huduma hiyo,” amesema.

Awali, kabla ya huduma hiyo kuanza kutolewa wilayani hapo, Kayombo amesema iliwalazimu wananchi kutembea zaidi ya kilometa 73 kufuata huduma hiyo wilaya ya Kibiti.

Amebainisha kuwa halmashauri imejipanga kuendelea kutoa huduma bora za kijamii zikiwemo afya na elimu kwa wananchi wake.