Rugemalira sasa aibua wanasheria

Sababu kesi ya Rugemalira kufutwa

Muktasari:

  • Siku moja baada ya mfanyabiashara James Rugemalira kuachiwa huru, wanasheria wamependekeza yafanyike mabadiliko ya sheria ili kuweka muda wa ukomo wa upelelezi katika kesi zilizopo Mahakamani.
  •  

Dar es Salaam. Siku moja baada ya mfanyabiashara James Rugemalira kuachiwa huru, wanasheria wamependekeza yafanyike mabadiliko ya sheria ili kuweka muda wa ukomo wa upelelezi katika kesi zilizopo Mahakamani.

Pia, wamependekeza Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) apunguziwe nguvu ili kusiwe na mianya ambayo inasababisha watu kukaa mahabusu kwa muda mrefu na baadaye kuachiwa huru kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa ushahidi.

Rugemalira aliachiwa huru juzi baada ya DPP kuieleza Mahakama kwamba hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, akiwa amekaa mahabusu kwa siku 1,550 tangu aliposhtakiwa Juni 19, 2017.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), alikuwa akikabiliwa na mashtaka 12 ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo amefutiwa mashtaka chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kauli za wanasheria

Wakizungumzia kesi ya Rugemarila na jinsi ya kuzuia watu kukaa mahabusu muda mrefu na baadaye kuachiwa, wanasheria walisema sasa ni wakati wa kurekebisha sheria ili kuwe na muda maalumu ambao uchunguzi wa mashtaka utakamilishwa.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga alisema sheria inaweza kutamka kwamba upelelezi lazima ukamilike ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo mtuhumiwa aachiwe huru.

“Kama kuna muda fulani wa kuchunguza, timu ya uchunguzi ya DPP itakuwa serious (makini) kuchunguza kesi husika. Sheria ikisema upelelezi lazima ukamilike ndani ya miezi mitatu kwa mfano, siyo mbaya,” alisema mwanasheria huyo.

Henga alisema suala la Rugemalira lina machungu nusu na furaha nusu, kwa maana kwamba watu wanafurahi kwamba ametoka na kuungana na familia yake, lakini machungu ni kwamba amekaa miaka minne gerezani halafu mtu anasema hana nia ya kuendelea na kesi.

“Tunachotaka sisi ni due process of the law (kufuata sheria), hata kama alikuwa na makosa. Huwezi kuendelea kufanya makosa juu ya makosa,” alifafanua mkurugenzi huyo wa LHRC.

Kwa upande wake, mwanasheria Alloyce Komba alisema ni muhimu kuwe na ukomo wa upelelezi kwa kila kesi inayofikishwa mahakamani, ili kuepusha watu kukaa mahabusu kwa muda mrefu wakati hawana hatia.

“Tunataka upelelezi wa kesi zote za uhujumu uchumi na kesi nyingine uwe na ukomo. Hii itapunguza mwenendo wa watu kushikiliwa mahabusu kwa muda mrefu kwa kisingizio kwamba upelelezi haujakamilika,” alisema.

Mwanasheria huyo alisema madaraka ya DPP ni makubwa, hivyo, anapendekeza yapunguzwe ili kuondoa mianya ya ukandamizaji wa haki za binadamu kupitia nafasi hiyo.

Komba aliongeza kwamba mashitaka ya jinai hayatakiwi kuvunja Katiba ya nchi, lakini kwa mwenendo wa kesi ya Rugemalira, Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilivunjwa.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea, Faraji Mangula alisema upelelezi unatakiwa kufanywa mapema, kabla mtuhumiwa hajakamatwa.

“Mtu akikamatwa wakati ushahidi haujakamilika, matatizo yake ndiyo kama haya ya Rugemalira, mtu anakaa mahabusu miaka minne ila hamna kitu chochote walichokikuta kwenye kesi yake,” alisema Mangula.

Rugemalira anaweza kushtaki

Akizungumzia uwezekano wa Rugemalira kuishitaki Serikali kwa kumweka mahabusu miaka minne kisha kukutwa hana hatia, Mangula alisema sheria inamruhusu kufungua mashtaka ya kuwekwa ndani.

“Anaweza kufungua kesi dhidi ya Serikali na watu wote waliokwenda kulalamika kwenye kesi. Wameshiriki kumweka ndani na kumnyima uhuru wake. Ipo sheria inaitwa Force Imprisonment, yaani kumweka mtu korokoroni bila kuwa na nia nzuri,” alisema.

Kwa upande wake, Wakili Komba alisema kesi ya Rugemalira imeonyesha kwamba kuna uvunjaji mkubwa wa haki zake na anaweza kushitaki wote waliohusika katika shauri hilo.

“Rugemalira amekaa ndani bila kosa lolote, DPP amethibitisha kwamba hana ushahidi wowote dhidi yake, ana uwezo wa kuishitaki serikali, kulishtaki Jeshi la Polisi, kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Komba.

Aliongeza kwamba DPP anachukua nguvu ya mahakama, kwa mfano kesi za uhujumu uchumi zinatakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu lakini zinapokuwa makahama za wilaya au mkoa, zinahitaji kibali cha DPP.