VIDEO: Rugemalira aanzia kanisani
Muktasari:
- Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara maarufu Tanzania, James Rugemalira.
Dar es Salaam. Saa chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru baada ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kueleza kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka yaliyokuwa yanamkabili, mfanyabiashara, James Rugemalira amekwenda katika Kanisa Katoliki Parokia ya Makongo Juu kumshukuru Mungu.
Akiwa ameambatana na ndugu na jamaa huku uso wake ukipambwa na tabasamu pana, Rugemalira aliyekuwa amevaa kanzu nyeupe alionekana akiimba nyimbo za kusifu na kuabudu alipokuwa kanisani hapo.
Mike Ngalo ambaye ni mwanasheria wa mfanyabiashara huyo ameieleza Mwananchi Digital leo Alhamisi Septemba 16, 2021 kwamba mteja wake amekwenda kanisani hapo kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa mema yote aliyomtendea.
Soma zaidi: Rugemalira afutiwa mashtaka, aachiwa huru