Sabaya afikishwa mahakamani tena kesi ya uhujumu uchumi

Sabaya afikishwa mahakamani tena kesi ya uhujumu uchumi

Muktasari:

  • Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30, tayari leo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha  kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi ambayo inamkabili na wenzake sita.



Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30, tayari leo Jumatano Oktoba 20, 2021 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha  kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi ambayo inamkabili na wenzake sita.

Sabaya amefika mahakamani saa 3:37 asubuhi leo 20, Oktoba akiwa ametulia huku akipungia mkono watu wachache ambao wamefika kusikiliza shauri lake.

Kesi ya Sabaya inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda na jamhuri inawakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Felix Kwetukia,Ofmed Mtenga na Wakili wa Serikali, Neema Mbwana.

Utetezi uliwakilishwa na mawakili, Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa, Fridolin Gwemelo, Edmund Ngemela na William Alexander.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27,2021 watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.