VIDEO: Sabaya kizimbani

New Content Item (1)
Sabaya kizimbani

Muktasari:

  • Aliyekuwa mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha leo mchana Ijumaa Juni 4, 2021 kujibu tuhuma zinazomkabili

Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha leo mchana Ijumaa Juni 4, 2021 kujibu tuhuma zinazomkabili.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi akiwa na walinzi wake sita na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine.

Sabaya kizimbani

Baada ya muda mfupi walichukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum wakisubiri kupelekwa mahakamani.

Kwa takribani wiki moja Sabaya alikuwa akihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma mbalimbali jijini Dar es Salaam.