Sabaya mgonjwa, kesi yaahirishwa

Sabaya mgonjwa, kesi yaahirishwa

Muktasari:

Kesi inayomkabili  aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,  Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Jumatano Agosti 4, 2021 imeahirishwa hadi kesho kwa kuwa Sabaya ni mgonjwa.

Arusha. Kesi inayomkabili  aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,  Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Jumatano Agosti 4, 2021 imeahirishwa hadi kesho kwa kuwa Sabaya ni mgonjwa.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana Jumanne  shauri la  Sabaya lilipangwa kuendelea kusikilizwa leo  ambapo shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Wilaya ya Arusha, ASP Gwakisa Minga alikuwa aendelee na ushahidi wake.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,   Odira Amworo,  mkaguzi msaidizi wa Magereza, Ramadhani Misanga ameieleza mahakama kuwa alipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa gereza kuu ya Arusha kuwa mshtakiwa wa kwanza (Sabaya) anaumwa hivyo hatoweza kufika mahakamani.

Hakimu Amworo amekubaliana na maombi hayo na kuahirisha kesi hadi kesho.