Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sabaya na wenzake wafikishwa tena mahakamani

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akisaidiwa kushuka kwenye karandinga mara baada ya kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi leo Agosti 12,2022. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi leo Agosti 12.

Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi leo Agosti 12.

Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya ofisi pamoja na rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa mfanyabishara wa Bomang'ombe, Alex Swai.

Washatakiwa wengine katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2022, ni pamoja na Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Sabaya alifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo Juni Mosi mwaka huu, ambapo awali kesi hiyo ilikuwa mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Janeth Joseph na Marryassumta Eusebi