Sabaya, wenzake huru

Muktasari:

  • Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi, pamoja na kutofautiana kwa mashahidi.

Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi, pamoja na kutofautiana kwa mashahidi.

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mbali na Sabaya, wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.

Hata hivyo,  Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Sabaya, wenzake wasubiri hukumu

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya rufaa yao kupinga kifungo cha miaka 30 jela. Soma zaidi