Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sabaya, wenzake kizimbani tena kesho

Muktasari:

  • Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne kesho Jumatatu Juni 20,2022  watafikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusikiliza   tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo uhujumu uchumi.





Moshi. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne kesho Jumatatu Juni 20,2022  watafikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusikiliza   tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo uhujumu uchumi.

Kesi hiyo namba mbili  ya mwaka 2022 inasikilizwa na  hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha na mawakili wanne  kutoka upande wa jamhuri ambao ni Tumain Kweka, Khalili Nuda, Verediana Mteuza na Suzy Kimaro.

Juni 7, 2022 hakimu Mshasha aliahirisha kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo Sabaya na wenzake walirudishwa katika gereza la Karanga.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Hata hivyo Juni 7,2022  wakati kesi hiyo ilipoitwa kutajwa wakili wa upande wa utetezi, Hellen Mahuna aliiomba mahakama hiyo kuharakisha upelelezi kwa kuwa mteja wake ambaye ni Sabaya ni mgonjwa kutokana na uvimbe alionao kichwani ambao anatakiwa kufanyiwa upasuaji.