Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la bandari lamuibua Dk Nshalla, azungumzia mabadiliko sheria ya uwekezaji

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Rugemeleza Nshalla

Muktasari:

  • Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Rugemeleza Nshalla amesema, kufuatia Muswada wa Sheria ya Uwekezaji iliyowasilishwa hivi karibuni bungeni, faida zinazotajwa kuwepo kwenye mkataba uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai hazina uhalisia.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Rugemeleza Nshalla amesema, kufuatia Muswada wa Sheria ya Uwekezaji iliyowasilishwa hivi karibuni bungeni, faida zinazotajwa kuwepo kwenye mkataba uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai hazina uhalisia.

Tayari Serikali imewahakikishia wananchi manufaa ya makubaliano hayo ambapo licha ya matarajio ya ongezeko la mapato kutoka Sh7 trilioni inayopatikana sasa, na kwamba baada ya uwekezaji uwekezaji wa Serikali ya Duabai kupitia kampuni ya DP World, utaongeza mapato kufikia Sh26 trilioni.

Juni 12, 2023 Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza na viongozi wa dini kuhusu mkataba huo wa awali amesema ufanisi mdogo wa bandari ndio sababu ya Serikali kutafuta uwekezaji.

Kuhusu mabadiliko ya sheria Dk Nshalla ameutaja muswada unaopendekeza sheria iliyotungwa mwaka 2017 kwa madhumuni ya kulinda rasilimali za nchi katika miradi ya uboreshaji na uendelezaji wa bandari inataka wananchi kushirikishwa kwenye maamuzi ya uwekezaji wa rasilimali za nchi.

Sheria hizo ni ile Mamlaka ya Nchi na Umiliki wa Rasilimali Asilia na Sheria ya Mapitio ya Majadiliano inayohusu Rasilimali na Maliasili za nchi Sura ya 450 zote za mwaka 2017.

"Madhumuni ya marekebisho hayo ni kuwezesha bandari katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia viwango vya kimataifa vya kiutendaji…kuvutia nchi nyingi zaidi na shehena kubwa za mizigo na kufanya uwekezaji wa bandari ya hapa nchini," imesema sehemu ya muswada huo.

Dk Nshalla amesema mabadiliko hayo ya sheria hayaruhusu uwazi kwenye rasilimali za bahari na maziwa na inamlinda mwekezaji jambo ambalo ni kinyume na Ibara ya 13(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo inaelekeza watu wote ni sawa na wana haki ya kulindwa.

"Sheria hii inayofanyiwa mabadiliko ya mwaka 2017 ilikuwa inaelekeza mikataba yote ambayo inaingiwa kwa namna ambayo inakuwa na manufaa kwa wananchi na mambo yataendeshwa kwa uwazi, sasa mabadiliko haya maziwa na bahari hayataendeshwa kwa uwazi,” amesema na kuongeza;

“Kwa nini watu wengine wabanwe alafu DP World wasibanwe, ni wazi faida zinazotajwa kuwepo kwenye mkataba huu ni za uongo."

Dk Nshalla amesema kutokana na ukosoaji wake kwenye mkataba wa DP World ameanza kupokea vitisho hata hivyo amevipuuzia huku akisema: “Siogopi, nitaendelea kusimamia katika msimamo huu.”